EVERTON YAIVUTA SHATI ARSENAL LIGI KUU ENGLAND

EVERTON yaivuta shati Arsenal ndani ya Ligi Kuu England baada ya kuwatungua kwenye mchezo wao walipokutana.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Goodison Park ulisoma Everton 1-0 Arsenal ambao ni vinara wa ligi.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo lilipachikwa kimiani na James Tarkowski dakika ya 60.

Huo ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha mpya wa timu hiyo Sean Dyche ambaye amepewa kazi hivi karibuni mara baada ya kutimuliwa kwa Frank Lampard.

Sasa Everon wanafikisha pointi 18 nafasi ya 17 huku ukiwa ni mchezo wa pili kwa Arsenal kupoteza msimu huu baada ya awali kupoteza mbele ya Manchester United.