MANULA KATUNGULIWA SIMBA IKISEPA NA POINTI TATU

KIUNGO wa Simba Pape Sakho amefunga bonge moja ya bao dhidi ya Singida Big Stars dakika ya 63.

Bao hilo linafanya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 3-1 Singida Big Stars.

Mabao mawili ya awali kwa Simba ni mali ya Jean Baleke aliyepachika bao mapema dakika ya 8 na lile la pili ni mali ya Saidi Ntibanzokiza dakika ya 20.

Singida Big Stars bao lao matata na zuri limefungwa na Bruno Gomez dakika ya 34 kwa pigo la faulo lilimshinda Aishi Manula.

Manula hakuwa na bahati na Gomez ambaye amefunga mabao 9 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Gomez kazitungua timu 8 ambapo kwenye mechi saba zote Singida Big Stars ilikuwa inasepa na ushindi lakini leo ngoma imekuwa nzito.