MSAFARA wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala umefika salama makao makuu ya Tanzania, Dodoma kwa walima Zabibu.
Azam FC kesho Januari ina kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Ni msafara wa wachezaji 24 ambao wamejumuishwa kwenye kikosi hicho ikiwa ni pamoja na Prince Dube, Ali Ahamada,Dube.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa wana kazi ngumu ya kufanya kwa ajili ya kusaka pointi tatu ugenini.