Home Sports KOCHA WA SIMBA KUANZA NA KIGONGO HIKI HAPA

KOCHA WA SIMBA KUANZA NA KIGONGO HIKI HAPA

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ametua ndani ya ardhi ya Dar baada ya kuibukia Brazil ambapo alikuwa na masuala ya kifamilia.

Kocha huyo ambaye amepewa mikoba ya Zoran Maki ameiongoza timu hiyo kwenye mechi mbili ilikuwa Simba 3-2 Mbeya City na Dodoma Jiji 0-1 Simba.

Kigongo kinachofuata ni dhidi ya Singida Big Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 3,2023.

Pia ana kazi ya kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika Simba ikiwa ipo hatua ya makundi.

Simba imepangwa kundi C ikiwa na timu ya Horoya ya Guinea,Vipers ya Uganda na Raja Casablanca ya Morocco

Ni Januari 24 alisepa Bongo usiku hivyo anarejea kuendelea pale alipoishia.

Ni mchezo mmoja hakuwa benchi ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho na Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Sadio Kanoute.

Previous articleASANTE JANUARI, KARIBU MWEZI WA UPENDO
Next articleMBRAZIL ATUA NA MIKWARA MIZITO SIMBA