UWANJA wa Mkapa dakika 45 za mwanzo ubao unasoma Yanga 5-0 Rhino Rangers.
Ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora ambapo mshindi atatinga hatua ya 16 bora na Yanga ni mabingwa watetezi.
Vijana wa Rhino Rangers wameshuhudia mabao hayo dakika ya 7 kupitia kwaDickson Ambundo, Kennedy Musonda dakika ya 15, Aziz KI dakika ya 19, Yannick Bangala dakika ya 26 n kiungo Farid Mussa dakika ya 24.
Kwa sasa ni mapumziko hivyo kuna kazi nyingine kwa Yanga na Rhino Rangers ndani ya dakika 45 zijazo.