Home Uncategorized TRY AGAIN: SIMBA HATUTAKUWA WANYONGE TENA, FURAHA INARUDI

TRY AGAIN: SIMBA HATUTAKUWA WANYONGE TENA, FURAHA INARUDI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Salim Abdallah, ‘Tryagain’ amesema kuwa kwa namna ambavyo timu hiyo imejipanga hawatakuwa wanyonge tena bali furaha itakuwa ni mwendelezo.

Hayo ameyasema leo kwenye mkutano wa Simba ambao una ajenda 13 ikiwa ni pamoja na ile ya uchaguz mkuu unaotarajiwa kufanyika leo Januari 29,2023.

Kiongozi huyo amesema:-“Nawashukuru wanachama na mashabiki wetu, tumepitia kipindi kigumu lakini mmeendelea kuwa nasi. Kwa niaba ya bodi tunawashukuru sana.

“Sasa tupo namba 10 Afrika kwa ubora wa vilabu. Tupo katika mapambano ya ligi, ligi ni ngumu lakini sisi viongozi tumejipanga timu yetu kupambana na mwaka huu kushinda ubingwa.

“Haya mafanikio hayakuja kwa bahati mbaya, sina budi kumshukuru Mo Dewji kwa upendo wake, ametumia pesa zake, muda wake, nguvu yake kuhakikisha tunayafikia mafanikio haya. Tuendelee kumtia moyo, amefanya kazi kubwa.

“Hivi karibuni tutapokea ujumbe kutoka FIFA na CAF kuja kukagua kama mnavyojua Simba ndio timu pekee kutoka ukanda wa CECAFA ambayo itashiriki Super Cup.

“Sina budi kumshukuru CEO aliyepita, amefanya kazi kubwa. Nachukua nafasi hii kumshukuru na namuombea dua katika changamoto yake mpya.

“Sasa kila mchezaji mkubwa Afrika anataka kuja kucheza Simba. Nawahakikishie Simba ile ya furaha inarudi, hatutakuwa wanyonge tena, Simba hii ni ya kimataifa.

“Nimepokea mwaliko mwingine kwenda kwenye semina ya FIFA kule Morocco. Hii ni kwa ajili ya Simba. Katika watu watatu Afrika mimi ni mmoja wao kwenda kuwawakilisha.”

Previous articleVIDEO:COASTAL UNION WALIKUWA IMARA,KUHUSU MANZOKI IPO HIVI
Next articleYANGA 5-0 RHINO RANGERS