Home Uncategorized VIUNGO HAWA WA SIMBA LAZIMA WAONGEZE UMAKINI KWA MIKATO YAO

VIUNGO HAWA WA SIMBA LAZIMA WAONGEZE UMAKINI KWA MIKATO YAO

HAWA viungo wote wa Simba hawana ujanja wa kuyeyuha dakika 90 bila kutembeza mikato yao jambo ambalo linaigharimu timu kwenye mechi wanazocheza na kuwagharimu wachezaji wa timu pinzani.

Sadio Kanoute, mtata akiwa ndani ya uwanja na kucheza faulo kwenye harakati za kuokoa mpira haoni tabu kutokana na asili ya eneo lake.

Nyota huyo alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kutokana na adhabu ya kadi ya njano hivyo ana kazi ya kuanza mwanzo upya na kwa umakini.

Mzawa Mzamiru Yassin hakati tamaa muda wote anakuja hachoki yeye na mpira anafunga anatengeneza pasi za mabao.

Alikosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji kutokana na adhabu ya kadi ya njano.

Angalau kidogo Jonas Mkude lakini yeye huwa anajijengea kautawala kake eneo atakalochagua hapo ukimfuata lazima akutemezee mikato ya kimyakimya.

Mkongwe huyu ni moja ya viungo wenye uwezo mkubwa lakini kwa sasa benchi limekuwana ushkaji naye mara kwa mara.

Kuna ingizo jipya eneo la kiungo mkabaji anaitwa Ismail Sawadogo hana jambo dogo mchezo wake wa kwanza tu kaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 60 akitumia dakika 71.

Kutokana na mikato yao ni lazima waongeze umakini wanapotimiza majukumu yao ili kuwalinda wachezaji wenzao kwani sio jambo jema kuwahezea faulo ambazo hazina ulazima.

Previous articleVIDEO;JEMBE AFUNGUKA ISHU YA FEI TOTO NA KESI YAKE
Next articleBALOTEL AINGIA ANGA ZA MPAPPE