Home Uncategorized MBRAZILI SIMBA AMPA BALEKE SAA 48

MBRAZILI SIMBA AMPA BALEKE SAA 48

KIKOSI cha Simba jana Jumanne kilirejea kambini baada ya mapumziko ya siku moja, huku Kocha Mkuu Mbrazili, Robert Olvieira ‘Robertinho’ akitenga programu ya siku mbili sawa na saa 48, kwa mastaa wote akiwemo straika Jean Baleke.

Lengo ni kuhakikisha Simba wanaibuka na ushindi dhidi ya Coastal Union na kukata tiketi ya kucheza robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Simba Jumamosi wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Coastal Union katika mchezo wa raundi ya tatu ya mashindano hayo, mchezo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mshindi wa mchezo huo atafuzu kuwa sehemu ya timu nane ambazo zitakuwa zimefanikiwa kukata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Robertinho kwa sasa ameondoka ndani ya kikosi cha Simba na kurejea kwao Brazil ambapo ana matatizo ya kifamilia na anatarajia kurejea baadaye mwezi huu kuendelea na majukumu yake Msimbazi.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Baada ya kuwa na mapumziko ya siku moja mara baada ya ushindi katika mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji kikosi leo (jana), Jumanne kinatarajiwa kurejea kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Coastal Union.

“Tunatarajia wachezaji wote wataripoti kwenye mazoezi hayo yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Simba MO Arena.”

Previous articleFEI TOTO AMPASUA KICHWA NABI YANGA
Next articleSINGIDA BS YAISHTUKIA YANGA KWA GOMES