KWENYE chati ya ufungaji mabao ndani ya Azam FC, Idris Mbombo ni namba moja akiwa ametupia mabao 7 kibindoni.
Nyota huyo ni imara kwenye mapigo huru ikiwa ni pamoja na penalti aliwahi kuwatungua Ruvu Shooting bao moja Uwanja wa Mkapa.
Hakuwa kwenye mwendelezo wake bora kutokana na kutokuwa fiti lakini kwa sasa ameanza kurejea mdogomdogo.
Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, Kali Ongala ameweka wazi kwamba kwenye upande wa ushambuliaji bado makali hayajaonekana sana kutokana na kushindwakutumia nafasi wanazopata.
“Kwenye ushambuliaji bado hatujawa imara sana lakini kuna mabadiliko hasa pale ambapo tunatengeneza nafasi hivyo kuzitumia ni jambo lingine ambalo ni muhimu kufuata.
“Unapozungumzia mpira kwa vijana hawa hauwezi kufanya mabadiliko mara moja ni hatua hivyo nina amini watakuwa imara na tutafunga,”.
Januari 23,2023 ubao wa Uwanja wa Liti ulisoma Singida Big Stars 1-0 Azam FC.
Katika mchezo huo nyota huyo hakuanza kikosi cha kwanza badala yake alianza benchi.