MCHEZO WA KIPA SIMBA KUBUMA AZAM FC HUYU HAPA MTIBUAJI

MABOSI wa Azam FC walikuwa kwenye hesabu za kuinasa saini ya kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya.

Dili hilo ghafla lilitibuka baada ya ya mabosi hao kupata zali la kipa mwingine ambaye walikuwa wakimfuatilia.

Ikumbukwe kwamba kwenye dirisha dogo Azam FC imefanya usajili wa mchezaji mmoja pekee huku idara nyingine ikiwa ni ushambuliaji na kiungo ikibaki vilevile kama ilivyo kwa upande wa mabeki.

Jina la Kakolanya linatajwa liliwekwa kando baada ya kumnasa kipa mahiri kutoka Ghana ambaye alitambulishwa kwa mashabiki wa Azam FC Januari 8,2023 wakati timu hiyo ilipokuwa inashiriki Kombe la Mapinduzi 2023.

Taarifa ya Azam FC ilieleza namna hii:”Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefanikiwa kumsajili kipa mahiri kutoka Ghana, Abdulai Iddrisu, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bechem United ya kwao Ghana,”.

Kipa huyo bado hajaanza kuonyesha makeke yake na badala yake amekuwa benchi akimshuhudia kipa namba moja Ali Ahamada akitimiza majukumu yake.

Januari 23 2023 Uwanja wa Liti alikuwa shuhuda wa bao la Bruno Gomes akiwa nje kidogo ya 18 wakati ubao ukisoma Singida Big Stars 1-0 Azam FC.