Home Sports YANGA YAKOMBA POINTI ZA RUVU SHOOTING

YANGA YAKOMBA POINTI ZA RUVU SHOOTING

56 ni pointi ambazo wanazo kibindoni Yanga baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting.

Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 umesoma Yanga 1-0 Ruvu Shooting na kuwafanya wayeyushe pointi tatu mazima.

Ni Mpoki Mwakinyuke ambaye ni nyota wa Ruvu Shooting alijifunga kwenye harakati za kuokoa hatari langoni mwake.

Kipa wa Ruvu Shooting, Kahaki hakuwa na chaguo zaidi ya kushuhidia nyavu zikitisika na pointi zikisepa mazima.

Yanga inajikita kileleni ikiwa imecheza mechi 21 huku Ruvu Shooting iliyofunga mabao 10 baada ya kucheza mechi 21 inabaki na pointi zake 14.

Mzunguko wa kwanza Yanga iliwatungua Ruvu Shooting mabao 2-1 na sasa imewatungua bao 1-0 na kusepa jumla na pointi zote sita mbele ya Ruvu Shooting inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata.

Previous articleKMC V NAMUNGO FC KESHO KINAWAKA
Next articleMCHEZO WA KIPA SIMBA KUBUMA AZAM FC HUYU HAPA MTIBUAJI