YANGA YAMUANDIKIA BARUA FEI TOTO, WATAALAMU KUJADILI KIDOGO

SAKATA la nyota wa Yanga, Feisal Salum na mabosi wake Yanga bado halijafika mwisho ambapo waajiri wake hao wameweka wazi bado mchezaji ni mali yao.

Fei aliwashukuru Yanga na kuweka wazi kuwa anahitaji kupata changamoto nyingine kwa kile kilichoelezwa kuwa amevunja mkataba na kurejesha fedha ambazo zilikuwa zinahitajika kwa mujibu wa mkataba wake.

Kesi hiyo ilipelekewa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwenye Kamati ya Hadhi na Wachezaji ambapo iliamuriwa kwamba Fei bado ni mali ya Yanga na anapaswa kurejea kamini.

Yanga imemuandikia barua Feisal Salum kurejea kambini mara moja, hivi karibuni kamati imeadikiwa barua ya kuomba review kuhusu kesi yake  na wanasheria kuhusu hukumu ya nyota huyo.

Kisheria watu wakiwa bado na kesi, inawezekana vipi mchezaji akarejea kazini au anatakiwa kurejea baada ya kesi kwisha?

Kuwasilisha kwa REVIEW, maana yake upande mmoja haujakubali hukumu…ni sawa mchezaji arejee huku akiwa na kesi na klabu?

Binafsi naendelea kufuatilia kujua FIFA wanaagiza nini katika hili..

WATAALAMU tupeni mafunzo kisheria….Fei anapaswa KUREJEA sasa au ATAREJEA au KUONDOKA kesi itakapofikia tamati? Swali la Jembe