Home Sports WAZAWA ONYESHENI THAMANI ILE MNAYOSTAHILI

WAZAWA ONYESHENI THAMANI ILE MNAYOSTAHILI

IMEKUWA ngumu kwa wachezaji wazawa kuwa kwenye mwendelezo bora kila wakati haina maana kwamba hawawezi hapana inaonekana wanakata tamaa mapema.

Kwa sasa ukitazama kwenye kila idara wale ambao wanafanya vizuri ni wachezaji wakigeni hakika hili ni jambo ambalo lazima liwashtue wazawa.

Angalau miaka ya hivi karibuni kwenye eneo la makipa wazawa walikuwa wanaonyesha ule uwezo wao kwenye kulinda lango lakini sasa imekuwa tofauti.

Kwenye eneo la viungo na washambuliaji bado wageni wanashika nafasi kubwa na kuendelea kutangaza bendera za nchi yao kwenye ardhi ya Tanzania.

Hakika kwa mwendo ambao wanazidi kwenda nao kama wazawa hawatashtuka itakuwa ngumu kufanikiwa kuwa wenye ushindani nao.

Soko litaanza kuwa gumu kwa wachezaji wazawa sio kwamba watakuwa hawana uwezo bali namba zitakuwa zinawahukumu.

Itakuwa kila wakala akitaka kuuliza bei ya mchezaji nakutazama rekodi lazima atakuwa na maswali ya gharama atakayotajiwa jambo litakalofanya achague gharama ambayo atakuwa anahitaji yeye.

Inawezekana wazawa kushindana na wageni kwani wote mnashiriki ligi moja na kila mbinu ambazo wanazitumia mnaziona.

Basi ni wakati wenu kufanya kazi kwa bidii huku mkiendelea kujituma bila kukata tamaa.

Muda ni sasa na sio mpaka kusubiri kesho mambo yatakuwa yamebadilika pale ambapo mtaamua kuchukua maamuzi jioni.

Kila la kheri kwenye majukumu yenu na ushindani ni muhimu kuendelea lakini nanyi lazima muonyeshe thamani yenu kwa vitendo.

NB:Picha haina tafsiri ya hukumu kwa wachezaji hapana ni picha kama zillivyo picha nyingine.

 

Previous articleYANGA YAMUANDIKIA BARUA FEI TOTO, WATAALAMU KUJADILI KIDOGO
Next articleBRUNO AWATULIZA MATAJIRI WA DAR