BAO pekee la ushindi kwenye mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Mkapa limepachikwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Ubao umesoma Dodoma Jiji 0-1 Simba ambapo ni bao la Jean Baleke aliyetumia pasi ya Kibu Dennis.
Shukran kwa Baleke ambaye alikuwa na utulivu ndani ya 18 huku makosa ya safu ya ulinzi ya Dodoma Jiji yakiigharimu timu hiyo.
Daniel Mgore kipa wa Dodoma Jiji hakuwa na chaguo kwenye mchezo huo na kushuhudia nyavu zake zikitikisika muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko.
Dodoma Jiji walikuwa wanapenya kwenye safu ya ulinzi ya Simba kwa urahisi walichokosa ilikuwa kwenye umaliziaji kupitia kwa Hassan Mwaterema na Collins Opare.
Simba inafikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 21 huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 53 na wamecheza mechi 20.