Home Uncategorized MASHINE MPYA SIMBA KUANZA NA DODOMA JIJI

MASHINE MPYA SIMBA KUANZA NA DODOMA JIJI

JUMA Mgunda, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wachezaji wote ambao wamesajiliwa kweye dirisha dogo wapo tayari kwa ajili ya kutimiza majukumu ndani a timu hiyo.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Robert Oliviera kwenye dirisha dogo ni wachezaji watatu wapya imewasajili ambao ni Jean Baleke, Ismail Sawadogo na Mohamed Mussa.

Jana walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mgunda amesema:”Wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha dogo wapo tayari kwa ajili ya kucheza na sio kwa ajili ya majaribio,”.

Wachezaji hao wapo na timu Dodoma hivyo wanatarajiwa kuweza kuanza kwenye mchezo wa leo Januari 22,2023.

Previous articleMUONEKANO WA UKURA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI
Next articleWAARABU WAINGIA ANGA ZA YANGA KUISAKA SAINI YA BEKI