Home Uncategorized MASHINE ZA KAZI YANGA KAMILI KWA RUVU

MASHINE ZA KAZI YANGA KAMILI KWA RUVU

AZIZ Ki kiungo wa Yanga ni miongoni mwa mastaa ambao wameanza mazoezi kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumatatu, Uwanja wa Mkapa Januari 23,2023.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa wameweka kibindoni pointi 53 kwenye mechi 20 ambazo wamecheza wamepoteza mchezo mmoja pekee.

Mbali na Aziz KI pia Yannick Bangala, Kennedy Musonda, Dickosn Job, Clement Mzize ni miongoni mwa waliokuwa kwenye mazoezi hayo.

Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao watapambana kupata matokeo.

Previous articleMBRAZIL WA SINGIDA BIG STARS YEYE ANATUPIA TU
Next articleSIMBA YATAMBA, KINATOKA CHUMA KINAINGIA CHUMA