Home Uncategorized YANGA MIPANGO YAO IPO HIVI

YANGA MIPANGO YAO IPO HIVI

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikubwa ambacho amewaambia wachezaji wake ni kucheza kwa umakini kila mechi.

Timu hiyo imekuwa kwenye mwendo bora msimu huu ambapo imepoteza mchezo mmoja kati ya 20 kibindoni ina pointi 53.

Mchezo wake wa fungua mwaka ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo wapinzani wao walionekana kutumia mbinu ya kujilinda zaidi.

Bao la ushindi lilifungwa na Fiston Mayele ambaye anafikisha mabao 15 kwenye ligi akiwa ni namba moja kwa utupiaji anafuatiwa na Moses Phiri wa Simba mwenye mabao 10.

Nabi anafanya kazi kwa kushirikiana na Cedrick Kaze ambaye ni msaidizi wake wakiwa ndani ya Jangwani.

“Kila mchezo kwetu ni mgumu na tunawaambia wachezaji kuwa kazi yetu ni kusaka ushindi nao wanaelewa kisha tunapata matokeo,”.

Timu hiyo kwa sasa imeanza maandalizi kuelekea mchezo wake wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa Januari 21,2022 Uwanja wa Mkapa.

Previous articleRIPOTI KUAMUA HATMA YA TAMBWE, KAGERE, SINGIDA BIG STARS
Next articleNABI AWACHAMBUA MAYELE, MUSONDA,MFUMO WABADILISHWA SIMBA