Home Sports JEMBE JIPYA YANGA LAANZA MAZOEZI

JEMBE JIPYA YANGA LAANZA MAZOEZI

BAADA ya kukamilisha usajili wake ndani ya kikosi cha Yanga, hatimaye kipa namba mbili wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ameanza mazoezi.

Ni Metacha Mnata ambaye alikuwa anakipga ndani ya Singida Big Stars iliyogotea nafasi ya pili hatua ya fainali kwenye Kombe la Mapinduzi 2023.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Januari 13, Mnata alikuwa langoni na ametambulishwa Yanga kuanza changamoto mpya.

Januari 17,2023 kipa huyo ameanza mazoezi na wachezaji wenzake ambao wametoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Ihefu mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa Januari `16,2023 kwa bao la Fiston Mayele dakika ya 63 akitumia pasi ya Jesus Moloko.

Mbali na Mnata pia mwamba mwingine ambaye ameanza kazi ni kipa wa makocha raia wa Brazil, Milton Nienov ambaye hakuwa na timu hiyo kwa muda alipokuwa nchini Brazil.

Kocha huyo ambaye aliwahi kufanya kazi kwa watani za jadi Simba kwa kumnoa Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salim kwa sasa anawanoa makipa wa Yanga ikiwa ni pamoja na Djigui Diarra,Aboutwalib Mshery na Eric Johora.

Mchezo ujao wa Yanga kwenye Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Januari 21,2023.

Previous articleVIDEO:WILSON OURUMA AWAVAA YANGA
Next articleWIKI HII NI USHINDI TU MERIDIANBET KWA ODDS BOMBA, AC MILAN DHIDI YA INTER MILAN KITAWAKA!