Home Sports MNYAMA KUSHUSHA CHUMA KINGINE

MNYAMA KUSHUSHA CHUMA KINGINE

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa bado haujamaliza usajili na kabla ya dirisha dogo kufungwa watashusha chuma cha kazi kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho.

Simba kwa sasa ipo Dubai kwa ajili ya kambi ambayo itatumia siku 7 ikiwa ni mualiko maalumu kutoka kwa Rais wa heshima wa timu hiyo Mohamed Dewji, ‘Mo’.

 Ahmed Ally, meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, amesema kazi bado inaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji.

“Hatujamaliza usajili kuna wachezaji ambao tupo nao kwenye mazungumzo ikiwa tutafikia nao makubaliano tutawatambulisha kwa mashabiki na wanachama hivyo wasiwe na presha.

“Hatuwezi kuwataja kwa muda huu kwa kuwa bado usajili unaendelea na ukimtaja unayemtaka zipo timu ambazo zitamfuata na kuharibu mipango hivyo ni suala la kuwa na subira katika hilo,” amesema Ally.

Ni Saidi Ntibanzokiza alikuwa anakipiga Geita Gold sasa ni mali ya Simba ni usajili wa kwanza kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Previous articleODDS NONO KWENYE DABI ZA KIBABE EPL & SERIE A! BASHIRI POPOTE, WAKATI WOWOTE!
Next article32 BORA SIMBA, YANGA NA AZAM WAWAJUA WAPINZANI WAO