Home Sports NYOTA KIBU AMKOSHA KOCHA MPYA SIMBA

NYOTA KIBU AMKOSHA KOCHA MPYA SIMBA

ROBERT Oliviera Kocha Mkuu wa Simba amekoshwa na maufundi ya mshambuliaji wa timu hiyo Kibu Dennis.

Katika mazoezi yaliyofanyika jana Januari 11, raia huyo wa Brazil alimchangua Kibu kuwa mchezaji bora wa siku hiyo na kumpa zawa.

Kibu alikabidhiwa zawadi hiyo mbele ya wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha John Bocco mwenye mabao 9 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Wakiwa nchini Dubai ambapo wameweka kambi kwa muda wameanza mazoezi wakiwa na kocha mpya akishirikiana na Juma Mgunda ambaye ni mzawa.

Kocha huyo amesema:”Nimefurahishwa na uwezo wa wachezaji wote kutokana na kuwa na vipaji lakini Kibu amenifurahisha uwezo wake jambo ambalo limefanya nimpe zawadi.

“Nina amini kwamba wachezaji wote watakuwa na kazi kubwa kwenye mechi zetu zijazo lakini kwa sasa tunafanya maandalizi ambayo yatatufanya tuwe imara,”.

Previous articleYANGA YAIVUTIA KASI IHEFU
Next articleODDS NONO KWENYE DABI ZA KIBABE EPL & SERIE A! BASHIRI POPOTE, WAKATI WOWOTE!