SIMBA YAKWEA PIPA, BANDA,NTIBANZOKIZA NDANI

NYOTA wa Simba Peter Banda tayari amerejea kwenye ubora wake akiwa ni miongoni mwa mastaa waliokwea pipa kuelekea Dubai.

Kikosi hicho kimepata mualiko maalumu kutoka kwa Rais wa Heshima Mohamed Dewji ambapo kitaweka kambi kwa muda wa siku 7.

Wengine ambao wapo kwenye kikosi hicho ni pamoja na Said Ntibanzokiza, Sadio Kanoute huku Moses Phiri yeye ataunganisha safari akitokea Zambia kama ilivyo kwa Clatous Chama.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wanaamini kambi hiyo itakuwa na matokeo mazuri.

“Kwa sasa tunafikiria kuhusu Dubai na tunakwenda huko na benchi la ufundi kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu za ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika,”.