Home Sports YANGA WAKIWASHA KOMBE LA MAPINDUZI USIKU KABISA

YANGA WAKIWASHA KOMBE LA MAPINDUZI USIKU KABISA

WAKATI watani zao wa jadi Simba wakifungua mwaka 2023 kwa kunyooshwa na Mlandege kwenye Kombe la Mapinduzi, Yanga wao wameanza kwa ushindi.

Katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya KMKM uliochezwa Uwanja wa Amaan ubao uligoma kubadilika katika dakika 90 za kawaida.

Ilibidi Yanga wasubiri mpaka dakika ya 90+5 na kupata bao la ushindi kupitia kwa nyota wao Dickson Ambundo.

Katika mchezo huo nyota Zawad Mauya wa Yanga alichaguliwa kuwa mchezaji mwenye nidhamu huku kipa wa KMKM akiteuliwa kuwa mchezaji bora wamchezo huo.

Kwenye mchezo huo Yacouba Songne na Mudathir Yahya walianzia benchi kuusoma mchezo na walipoingia kila mmoja alionyesha makeke yake.

Yacouba alikuwa mzuri kwenye kupandisha mashambulizi na kutengeneza nafasi ambazo hazikutmiwa na washambuliaji wa Yanga waliokuwa wakiongozwa na Ambundo eneo la kati.

Previous articleSLOTI YA EXPANSE KASINO NA MERIDIANBET USHINDI MKONONI MWAKO!!
Next articleKAZI IMEANZA, MBRAZIL AIFUMUA SIMBA, NABI ATOA MAJUKUMU MAPYA