Home International PUMZIKA KWA AMANI LEGEND PELE

PUMZIKA KWA AMANI LEGEND PELE

GWIJI wa soka wa Brazil Pele, mmoja wa wachezaji bora zaidi wa wakati wote, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Mshambulizi huyo wa zamani, ambaye ndiye mchezaji pekee katika historia kushinda vikombe vitatu vya Kombe la Dunia, aliaga dunia katika hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo kufuatia kuugua saratani.

Pele, ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Brazil akiwa amefunga mabao 77 katika mechi 92, alikua kinara wa mchezo huo baada ya kushinda Kombe la Dunia mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 17, akifunga mabao mawili kwenye fainali na kuwashinda wenyeji Sweden.

Ujumbe kutoka kwa akaunti rasmi ya Twitter ya Pele siku ya Alhamisi ulisomeka: “Msukumo na upendo viliashiria safari ya Mfalme Pele, ambaye aliaga dunia kwa amani leo. Upendo, upendo na upendo, milele.”

Previous articleLIGI IMECHANGANYA, MECHI KALI ZA FUNGA MWAKA 2022 ZENYE ODDS KUBWA NA MACHAGUO KIBAO MERIDIANBET
Next articleVITA YA MATAJIRI, KAMA NOMA NA IWE, FEI AWACHENGA YANGA SC AIBUKIA JESHINI