Home Sports MZEE WA KUCHETUA NA ZANZIBAR FINEST KUIKOSA MTIBWA SUGAR

MZEE WA KUCHETUA NA ZANZIBAR FINEST KUIKOSA MTIBWA SUGAR

KUELEKEA mchezo wa funga mwaka kwa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar kiungo Bernard Morrison mzee wa kuchetua hatakuwa sehemu ya mchezo huo.

Utakuwa mchezo wa mwisho kwa timu zote mbili kucheza ndani ya 2022 tukisubiri Neema ya Mungu kuuanza 2023.

Sababu kubwa ya nyota huyo kutokuwa kwenye kikosi hicho ni kutokana na matatizo ya kifamilia.

Mshikaji wake Dickson Ambundo ni miongoni mwa nyota ambao wapo na kikosi Morogoro, mji kasoro bahari.

Yanga inatarajiwa kumenyana na Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Yanga ilisepa na pointi tatu Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa nyota ambao walifunga ni pamoja na beki Djuma Shaban ambaye pigo lake la faulo lilizama mazima kwenye nyavu za Faroukh Shikalo.

Nyota mwingine ambaye atakosekana kweye mchezo huo ni Feisal Salum ambaye suala la mkataba wake limekuwa na mvutano na mabosi wake hao.

Previous articleVIDEO: HIZI HAPA SABABU ZA YANGA KUWATAKA WACHEZAJI WA AZAM FC
Next articleHIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA PRISONS, NTIBANZOKIZA NDANI