NYOTA Abdul Seleman,’Sopu’ kiungo wa Azam FC ameanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa leo Desemba 25,2022 dhidi ya Yanga.
Ikumbukwe kwamba alipokuwa Coastal Union Sopu alifunga hat trick kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga jambo lililowavutia mabosi wa Azam FC.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ukisubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki hii Dabi ya Mzizima.
Kali Ongala ambaye ni Kocha Mkuu wa Azam FC ameanza na Ali Ahmada langoni pia wengine ni Lusajo Mwaikenda,Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Edward Manyama.
Yupo Kenneth Muguna, Prince Dube, James Akamiko, Kipre Junior.