RASMI uongozi wa Coastal Union umetangaza kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Yusuf Chipo ambaye alikuwa ni kocha mkuu wa timu hiyo.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Coastal Union leo Desemba 20,2022 imeeleza kuwa Desemba 19, 2022 walifikia makubaliano ya kusitisha mkataba huo kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Kwa sasa timu hiyo ambayo ina mchezo wa ligi dhidi ya Yanga itakuwa chini ya kocha msaidizi Joseph Lazaro.
Ikumbukwe kwamba Septemba 12,2022 Katibu Mkuu wa Coastal Union, Omar A.S Ayoub (kushoto) alimtambulisha kocha Yusuf Chipo kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Chipo alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo ambapo alichukua mikoba ya Juma Mgunda anayeinoa Simba