FAINALI YA KIBABE LEO KOMBE LA DUNIA

DESEMBA 18,2022 Fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022 inatarajiwa kufanyika leo Jumapili kwenye Uwanja wa Lusail Iconi.

Mataifa mawili yanakutana kumsaka mshindi atakayesepa na taji hilo kubwa duniani.

Mabingwa watetezi Ufaransa wenye Klylian Mbappe dhidi ya Argentina yenye Lionel Messi.

Argentina leo watacheza fainali yao ya sita kwenye Kombe la Dunia wakiwa wamepotezwa na Timu ya Taifa ya Ujerumani ambayo imecheza fainali mara nane.

Pia Argentina leo wanasaka taji la tatu baada ya kutwaa taji hilo mwaka 1978 na 1986 ikiwa watapoteza leo itakuwa ni fainali yao ya nne kunyooshwa.

Ufaransa wao wamefika fainali mara nne tangu mwaka 1998,2006,2018 na 2022 kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikifanya vizuri na ni mabingwa watetezi.

Mastaa wawili ambao wanacheza Klabu ya PSG, Messi na Mbappe hapa kila mmoja anapambania taji lake na heshima.

Messi mwenye miaka 35 yeye hana bahati ya kuvaa medali kwenye Kombe la Dunia ambapo Mbappe anayo moja.

Jumla Messi kacheza mechi 25 wakati Mbappe akiwa amecheza mechi 13 na kwa upande wa mabao Messi katupia jumla ya mabao 11, asisti 8 akiwa na wastani wa kufunga kila baada ya dakika 199 na Mbappe ni 9 na asisti mbili akiwa na wastani wa kufunga bao kila baada ya dakika 112