>

MWAMBA WA LUSAKA KAKIMBIZA NA HUKU PIA

CLATOUS Chama kiungo wa Simba amewafunika viungo wote ndani ya timu tatu zilizo ndani ya tatu bora kwenye kutoa pasi nyingi za mabao kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Shirikisho.

Vigogo Yanga, Azam hizi kweye ligi zinapambana kujenga utawala wao ambapo kinara wa pasi za mwisho ni Clatous Chama mwenye pasi 8 na mabao mawili akifuatiwa na Ayoub Lyanga wa Azam FC akiwa na pasi tano na bao moja huku Jesus Moloko akiwa nazo tatu.

Timu hizo kwenye Kombe la Shirikisho zote zimetinga hatua ya 32 kwa ushindi wa mabao zaidi ya 7, ambapo Azam FC iliyo nafasi ya tatu kwenye ligi ilishinda mabao 9-0 Malimao FC, Yanga ambao ni vinara kwenye ligi wao walishinda 8-0 Kurugenzi na Simba 8-0 Eagle.

Kwa vinara wa kutengeneza pasi za mwisho kwenye mechi hizo kwa upande wa viungo ni Chama ambaye anazo mbili na alifunga mabao mawili pia kisha anafuata Djuma Shaban mwenye pasi mbili lakini hajafunga na kwa upande wa Azam FC ni Abdul Suleiman, Sopu mwenye pasi moja na mabao mawili.

Hivyo Chama kwenye ulimwengu wakutengeneza pasi kwa upande wa viungo amewafunika kwa mara nyingine tena kwenye kombe la shirikisho ambapo mabingwa watetezi ni Yanga.