>

AZAM FC NI MOTO KWENYE LIGI

KWENYE timu ambazo zimefunga kwa rekodi matata ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 huwezi kuiweka kando Azam FC.

Licha ya mechi zake kuwa na ushindani mkubwa pamoja na adhabu kwa baadhi ya wachezaji kama ilivyotokea mchezo wa Azam FC 3-2 Coastal Union bado boli inatembea.

Ni Ayoub Lyanga huyu ni mtambo wa mabao akiwa na pasi tano za mabao kwenye ligi.

Bao lake moja alifunga kwenye mchezo wa kufungia mzunguko wa kwanza Uwanja wa Ushirika, Moshi dakika ya 15.

Azam FC inayonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala ilisepa na pointi tatu huku Ongala akiweka rekodi ya kuwa kocha aliyeiongoza timu hiyo kushinda kwenye mechi 8 mfululizo.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili na pointi zake ni 35 baada ya kucheza mechi 15.