SIMBA YAWATULIZA COASTAL UNION MKWAKWANI

 MCHEZO wa pili mfululizo kikosi cha Simba kinafanikiwa kushinda kwenye mechi za ligi baada ya leo Desemba 3,2022 kushinda mbele ya Coastal Union.

Ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, umesoma Coastal Union 0-3 Simba na wakasepa na pointi tatu mazima.

Mabao ya Moses Phiri dakika ya 53 na dakika ya 60 kwa mkwaju wa penalti yalifungwa kipindi cha pili na lile la tatu ni mali ya kiungo Clatous Chama.

Coastal Union walikuwa wakifanya mashambulizi wakiwa nje ya 18 kwa kuwatumia mastaa wao Mtenje Albano, Aboubhakar Vincent walikwama kuwatungua makipa wa Simba ambapo alianza Aishi Manula kipindi cha kwanza na kipindi cha pili alikaa langoni Beno Kakolanya,

Sadio Kanoute alionyeshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo wa leo na kuondolewa kwa kadi nyekundu.

Simba inafikisha pointi 34 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.