INAELEZWA kuwa miongoni mwa nyota ambao wataachwa ndani ya kikosi cha Simba hivi karibuni ni pamoja na beki wa kazi Mohamed Ouattara.
Huyo nibeki wa kati wa Simba ni miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwa kwenye mpango wa kuondolewa kikosini hapo kutokana na kushindwa kuonyesha makali yake.
Mbali na beki huyo ambaye alikuwani chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Zoran Maki aliyesepa ndani ya kikosi cha Simba pia Victor Ackapn naye maisha yanaokena kuwa magumu kwake.
Ackpan ambaye alivutwa ndani ya kikosi cha Simba akitokea Coastal Union hajawa fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.
Orodha inaendelea kutajwa kuwa hata mkongwe Erasto Nyoni yupo kwenye uangalizi mkubwa ikiwa atashindwa kufurukuta basi safari yake inaweza kugota ukingoni.
Mshambuliaji bora Kibu Dennis ambaye msimu wa 2021/22 alifunga mabao 8 na pasi nne naye pia anaweza kuachwa ikiwa hatarejea kwenye ubora wake.
Hivi karibuni, Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari ndani ya Simba aliweka wazi kuwa kwa sasa masuala ya usajili bado hivyo wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi.