AZAM FC HESABU KWA POLISI TANZANIA

VIJANA wa Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Kali Ongalakwa sasa wapo kwenye maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara zinazofuata ndani ya Desemba,2022.

Chini ya Ongala kwenye mechi 7 ambazo amekiongoza kikosi hicho hajapoteza mchezo akiwa amekusanya clean sheet nne bila kuambulia sare.

Kituo kinachofuata ni dhidi ya Polisi Tanzania, Desemba 5, Uwanja wa Ushirika, Moshi ambapo unatarajiwa kuwa mchezo wao 8.

Ongala ameweka wazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wanaamini kwamba watapata matokeo chanya kwenye mechi zijazo ndani ya ligi.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye maandalizi ya mchezo huo ni pamoja na Pascal Msindo, Ayoub Lyanga, Idris Mbombo, Nondo.

“Kila mchezaji anajua majukumu yake na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani, ligi ina ushindani na kila timu inahitaji kupata matokeo chanya,” amesema Ongala.

Polisi Tanzania imemtambulisha Mwinyi Zahera leo Desemba 2,2022 hivyo kibarua chake cha kwanza itakuwa dhidi ya Azam FC.