KWENYE droo ya Azam Sports Federation raundi ya pili ambayo imechezwa leo Novemba 30,2022 Simba imewatambua wapinzani wake.
Ni kikosi cha Eagle kitapambana na Simba kusaka ushindi kwenye mchezo wao huo ujao.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 9-11, 2022 ambapo Simba waliweka wazi kuwa wanahitaji kutwaa taji hilo.
Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunissia.