NYOTA Marcus Rasford alikuwa kwenye ubora wakati timu ya taifa ya England ikiwatungua mabao 3-0 Wales kwenye mchezo wa hatua ya makundi, Kombe la Dunia Qatar.
Ni dakika ya 50 na 68 nyota huyo alifunga huku bao lingine likiwa ni mali ya Phil Foden dakika ya 51 kwenye mchezo huo wa kundi B uliokuwa na ushindani mkubwa.
Mbele ya mashabiki 44,297 walishuhudia burudani hiyo na Wales walipata wakati mgumu kwenye mchezo huo kupata ushindi ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora Kombe la Dunia.
Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate ameweka wazi kuwa walikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na ushindani amao wamekutana nao jambo amalo linawafanya wazidi kupambana kwa mechi zijazo.
“Tulikuwa kwenye wakati mgumu kwa ambacho tumekipata ni muda wa kuendelea kupambana kwa ajili ya mechi zetu zijazo bado kazi ipo na tunaamini tutafanya vizuri kwenye mashindano haya,”.
England inamaliza ikiwa nafasi ya kwanza kwenye kundi B imekusanya jumla ya pointi 7baada ya kucheza mechi tatu na nafasi ya pili ipo mikononi mwa timu ya taifa ya Marekani ambayo ina pointi moja baada ya kukusanya pointi moja.
Baada ya England kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora watakutana na timu ya taifa ya Senegal kutoka Afrika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Desemba 4.