DAKIKA 90 zimekamilika Uwanja wa Ushirika Moshi na ubao umesoma Polisi Tanzania 1-3 Simba.
Simba walianza kufunga mabao yote hayo matatu ambapo kipindi cha kwanza walifunga mabao mawili kupitia kwa John Bocco dakika ya 332 na bao la pili ni Moses Phiri dakika ya 43.
Kipindi cha pili Polisi Tanzania waliongeza umakini na nguvu ya kushambulia kwa Simba wakimtumia Vitalis Mayanga ambaye aliyekuwa akiliandama lango la Aishi Manula.
Bao la tatu limefungwa na Phiri dakika ya 53 na lile la Polisi Tanzania limefungwa na Zuber Khamis dakika ya 90 akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Simba.
Nyota huyo amemtungua Air Manula katika dakika za lala salama likiwa ni bao la kufutia machozi kwa Polisi Tanzania.