MASHUTI mawili yalipigwa kwenye lango la Brighton na wapinzani wao Aston Villa na hayo yote yalijaa nyavuni.
Uwanja wa Falmer ulisoma Brighton 1-2 Aston Villla kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambao ulichezwa Novemba 13.
Ni mabao ya Danny Ings aliyefunga dakika ya 20 kwa mkwaju wa penalti na lile la pili alifunga mwenyewe dakika ya 54.
Bao la mapema la Brighton kupitia kwa Alexis Mac Allister dakika ya kwanza lilikwama kubakisha pointi tatu nyumbani.
Timu zote mbili zilipiga mashuti mawili yaliyolenga lango ambapo Aston Villa walipiga jumla ya mashuti 8 huku Brighton wakipiga mashuti 7.
Kwenye msimamo wapo nafasi ya 7 Brighton wakiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 14 huku Aston Villa wakiwa nafasi ya 12 na pointi 18 baada ya kucheza mechi 15.