AZAM FC wameibuka na ushindi wa maao 4-3 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Moro.
Kasi ya Azam FC ilianza kipindi cha kwanza ambapo walipata mabao yote hayo matatu yaliyowapa uongozi.
Ni Idris Mbombo ambaye ametupia mabao mawili dakika ya 18 na 30 kwenye mchezo huo wakiwa ugenini.
Bao la tatu ni mali ya Abdalah Kheri ambaye amefunga dakika ya 41 chini ya Kaimu Kocha Kali Ongala.
Msumari wa nne ulipachikwa na Daniel Amoah dakika ya 64.
Mtibwa Sugar walionyesha makali yao kwa kupata mabao mawili kupitia kwa Adam Adam dakika ya 61 na 75 kisha bao la tatu ni mali ya Nassoro Kiziwa dakika ya 76.
Soccer Football - International Friendly - Italy v Turkey - Stadio Renato Dall'Ara, Bologna, Italy - June 4, 2024 Turkey's Abdulkadir Omur shakes hands with Italy's Riccardo Calafiori after the match REUTERS/Daniele Mascolo