ARSENAL WASHINDA DARAJANI SASA NI NAMBA MOJA

WAKIWA Uwanja wa Stamford Bridge, Arsenal wamesepa na pointi tatu jumlajumla kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea.

Bao pekee la ushindi limefungwa kipindi cha pili baada ya dakika 45 za mwanzo ngoma kuwa nzito kwa wote.

Ni Gabriel amepeleka furaha Arsenal kwa kupachika bao hilo dakika ya 63 na kuwafanya mashabiki kushangilia kwa shangwe.

Ni namba moja tena kwenye kilele ndani ya Ligi Kuu England wakiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 13 wanafuatiwa na Man City wenye pointi 32 nao wamecheza mechi 13.

Chelsea ni nafasi ya 7 ikiwa na pointi 21 kwenye msimamo.