Home Sports RAIS YANGA AWAPA UHAKIKA KUTINGA MAKUNDI KIMATAIFA

RAIS YANGA AWAPA UHAKIKA KUTINGA MAKUNDI KIMATAIFA

RAIS wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa wanaimani ya timu hiyo kukamilisha mpango wa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Novemba 2,2022 Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain ya Tunisia, Uwanja wa Mkapa.

Injinia amesema:”Nataka niwahakikishie tutasonga mbele kwenda hatua ya makundi, siyo jambo baya kuumia kwa kitu unachokipenda lakini usiipende Yanga kisa inashinda ikifungwa siyo yako,” .

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wana wachezaji wazuri na imani ni kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na ligi.

Yanga imeangukia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya mpango wa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kukwama.

Iliondolewa kwa jumla ya mabao 2-1 Al Hilal ya Sudan na sasa inaendelea kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Previous articleWAARABU WAMBEBA MAYELE, BOSI SIMBA AMKINGIA KIFUA MGUNDA
Next articleMABAO MAKALI BONGO HAYA HAPA