Home Sports AZAM FC HAWANA HOFU KUZIKABILI SIMBA NA YANGA

AZAM FC HAWANA HOFU KUZIKABILI SIMBA NA YANGA

KALI Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wana uwezo mkubwa hivyo hawahitaji kupewa mambo mengi wa kuzikabili timu kongwe Bongo Simba na Yanga.

Msimu wa 2022/23 timu ya kwanza kuwatungua Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Juma Mgunda ni Azam FC ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni Prince Dube.

Ilipokutana na Yanga Uwanja wa Mkapa ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 hivyo waligawana pointi mojamoja.

Ongala amesema:” Kwa mechi ambazo zinawahusu Simba na Yanga, wachezaji wa Azam FC hawahitaji kuambiwa mambo mengi ni kukumbushwa tu, kazi ipo kwenye mechi nyingine jambo ambalo tunalifanyia kazi kwa sasa.

“Kila mmoja anajua wajibu wake na nimekuwa nikiongea nao mara kwa mara kuhusu umuhimu wa kupata matokeo. Tumeshinda mchezo wetu dhidi ya Simba tumefurahi lakini hatujashinda kitu bado kazi inaendelea kwa mechi ambazo zinafuata,” amesema.

Mchezo ujao ni dhidi ya Ihefu ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, kesho Oktoba 31.

Previous articleBRIGHTON YAICHAPA CHELSEA 4G
Next articleMERIDIANBET SOKA BONANZA NI NURU KWA VIPAJI VYA VIJANA