LICHA ya bao la kusawazisha ambalo lilifungwa na Idris Mbombo wa Azam FC dakika ya 18 bado pira kodi lilisepa na pointi tatu mazima.
Ni kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru baada ya dakika 90 ubao umesoma KMC 2-1 Azam FC.
Nyota wa KMC, Nzigamasab Styve alifunga bao la kuongoza dakika ya 15 kisha likawekwa usawa na Mbombo dakika ya 18 na kuwafanya waende mapumziko wakiwa wametoshana ngvu.
Kipindi cha pili George Makan’ga alipachika bao la ushindi kwa KMC dakika ya 57 ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.
Katika matokeo mengine Kagera Sugar imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Singida Big Stars.
Ni Amis Kizza alipachika bao dakika ya 15 kisha Bruno Gomes alicheka na nyavu mara mbili dakika ya 51 na 88.
Inakuwa ni siku mbaya kazini kwa mastaa wa Kagera Sugar na Azam FC kwa kuwa wamepoteza pointi tatu muhimu huku kicheko kikiwa kwa KMC na Singida Big Stars.