UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wachezaji wote waliopo kwenye kikosi hicho ikiwa ni pamoja na Moses Phiri, Clatous Chama, John Bocco, Kibu Dennis wanaandaliwa kwa ajili ya kupata ushindi dhidi ya Yanga.
Simba inatarajiwa kumenyana na Yanga kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kila mchezaji aliye kwenye kikosi hicho anajitambua jambo linalorahisha kazi kwa benchi la ufundi.
“Kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza tunapata nguvu ya kujiamini kutokana na kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa ikiwa ni Phiri,Chama, Bocco,Jonas Mkude, hawa hawatumii muda mwingi kufundishwa wanajielewa na wanafanya kazi.
“Tunajua tuna mechi na watani zetu wa jadi, (Yanga) kuna balaa zito linakwenda kufanyika na kila mchezaji anajua nini malengo yetu msimu huu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona burudani ya kweli,” amesema Ally.
Phiri anaongoza kwa washambuliaji wenye mabao mengi ndani ya ligi akiwa ametupia mabao manne msimu wa 2022/23.