Home International KIMATAIFA HAKUNA MUDA WA NYONGEZA MUHIMU KUJITUMA

KIMATAIFA HAKUNA MUDA WA NYONGEZA MUHIMU KUJITUMA

HAKUNA muda wa ziada kwenye maisha ya soka kwani hata ule ambao unakuwa unaogezwa unatokana na maamuzi ya mwamuzi wa kati kuangalia namna wachezaji walivyokuwa wakipoteza muda uwanjani.

Ipo hivyo kwa sasa wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano a kimataifa hawana muda wa kusema kwamba watasubiri mechi ya kwanza upindua meza hilo halipo.

Unakumbuka ile Simba iliyokuwa kwenye ubora yenye Clatous Chama, Luis Miquissone, John Bocco na Pascal Wawa pamoja na nyota wengine ambao walikuwa katika ubora?

Matumaini yao kutinga hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika yaligotea Afrika Kusini baada ya kufungwa na Kaizer Chiefs mabao 4-0 na kufanya mzigo kuwa mzito kwenye mechi ya pili Uwanja wa Mkapa.

Kumbe nini sasa cha kufanya ni kuamini kwamba hakuna muda wa kupoteza kwa wawakilishi hata kama watarudi kucheza nyumbani wanakazi kubwa kusaka ushindi.

Muda ni huu kimataifa kila mchezaji kufanya kweli kwa kutafuta ushindi kwenye mchezo wa kwanza unadhani nini kinatakiwa.

Tuna amini kwamba kwa namna hali ilivyo kila benchi la ufundi limepata muda wa kuwafuatilia wapinzani wao na kutambua namna gani watafanikiwa kupata ushindi.

Inaleta furaha kuanza kushinda mechi ya kwanza iwe nyumbani ama ugenini hii itaongeza nguvu ya kujiamini kwa mchezo wa pili.

Lakini hata Azam FC, Yanga ama Simba ikishinda haina maana kwenye mechi ya pili wapunguze kasi hapana iwe ni kazi kazi.

Previous articleSIMBA SC YAKODI DEGE LA KISHUA, NABI AITEGA AL HILAL
Next articleVIDEO:AGGY SIMBA AWACHAMBUA WAPINZANI WA YANGA