Home Sports IBRAHIM AJIBU ANAISHI ULIMWENGU WAKE

IBRAHIM AJIBU ANAISHI ULIMWENGU WAKE

STAA wa Azam FC, Ibrahim Ajibu anaishi kwenye ulimwengu wake ndani ya kikosi hicho kwa kuwa tangu amejiunga na matajiri hao wa Dar hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza.

Ajibu aliibuka Azam FC akitokea Simba aliahidi kuwa atafanya jitihada kutimiza majukumu yake ndani ya timu hiyo pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jambo ambalo limekuwa tofauti kabisa.

Msimu wake wa kwanza ndani ya Azam FC, alianza kikosi cha kwanza mechi nne na alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons akitokea benchi lakini msimu huu Azam FC hajaanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo hata mmoja.

Wakati ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine, kiungo huyo alikosekana kwa kuwa aliachwa Dar kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa ni za kiufundi.

Sababu zilizofanya akosekane kwenye mechi nne za awali zilielezwa kuwa ni majeraha aliyokuwa anasumbuliwa nayo mwanzo wa msimu.

Hakuwa kwenye kikosi kilichoshinda bao 1-0 dhidi ya Singida Big Stars, Oktoba 3 Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni mchezo wa sita wa ligi.

Hayupo kwenye orodha ya wachezaji 25 watakaolekea Libya kucheza mchezo wa kitaifa dhidi ya Al Khadar, unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi.

Sababu kubwa ya kutokuwa kwenye msafara huo ambao utaibukia Libya leo ni zile ambazo zimeelezwa kuwa ni za kiufundi.

Previous articleYANGA WAPATA HASIRA KIMATAIFA
Next articleVIDEO: UMESIKIA MKWARA WA KAMWE? YANGA NI KUBWA KULIKO AL HILAL