Home Sports MASTAA WAWILI GEITA KUIKOSA POLISI TANZANIA

MASTAA WAWILI GEITA KUIKOSA POLISI TANZANIA

 KITASA wa kazi ndani ya Geita Gold, Kelvin Yondani anatarajiwa kuukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi Polisi Tanzania.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Oktoba 4,2022, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Sababu kubwa ya kuukosa mchezo wa leo ni matatizo ya kifamilia ambayo anakabiliwa nayo.

Mbali na Yondani pia staa mwingine Ibrahim Seleman huyu aliumia kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo.

“Kelvin Yondan ana matatizo ya kifamilia ambayo alipata msiba, hivyo hataweza kucheza mchezo huo na Ibrahim Seleman yeye aliumia,”.

Mchezo uliopita wa ligi, Geita Gold ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji.

Previous articleMGUNDA KICHEKO SIMBA, YANGA SC YATEGUA MITEGO YA AL HILAL
Next articleCHAMA MGUU WAKE WA KULIA NI SHIDA TUPU