Home Sports SIMBA YA JUMA MGUNDA YAWEKA REKODI DK 180

SIMBA YA JUMA MGUNDA YAWEKA REKODI DK 180

 NDANI ya dakika 180, Zanzibar, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda ameshuhudia wachezaji wake wakishinda mechi zote mbili.

Kwenye mechi hizo Simba haijaruhusu bao la kufungwa huku ikifunga jumla ya mabao manne, moja ni kwa pigo la penalti.

Mchezo wa kwanza ilikuwa dhidi ya Malindi FC ambapo Simba ilishinda bao 1-0 huku mtupiaji akiwa ni mzawa Nassoro Kapama aliyetumia pasi ya Peter Banda.

Mchezo wa pili, Simba ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Kipanga kwenye mchezo uliochezwa jana, Septemba 28.

Mabao ya Simba yalifungwa na Augustino Okra ambaye alitupia mabao mawili dakika ya 36 na 59 huku moja likifungwa na Kibu Dennis.

Mchezo wa mwisho kwa Mzungu wa Simba, Dejan kucheza ilikuwa dhidi ya Malindi na hakuyeyusha dakika 90.

Previous articleAJIBU AACHWA DAR AZAM IKIWAFUATA TANZANIA PRISONS
Next articleVIDEO:MANDONGA MTU KAZI AMVAA MWAKINYO