DE GEA KAINGIA ANGA ZA JUVENTUS

IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Juventus ipo kwenye mpango wa kuwania saini ya kipa namba moja wa Manchester United, David de Gea.

Hesabu za Juventus ni kuinasa saini ya nyita huyo kwa ajili ya msimu ujao ili apate cangamoto mpya.

Mkataba wa kipa huyo ndani ya United unatarajiwa kugotea ukingoni mwishoni mwa msimu huu ingawa kuna kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Habari zinaeleza kuwa wakati Juventus wao jicho lao likiwa kwa De Gea, United wao wanamtazama kwa ukaribu Jordan Pickford kuwa mbadala wake.

Juventus wapo tayari kumsajili De Gea kuongeza nguvu mbele ya Wojciech Szceny, Mattia Perin na Carlo Pinsoglio ambao wapo kikosini hapo kwa sasa.