Home Sports USHINDI UWE NA MWENDELEZO KIMATAIFA KWA TIMU ZA TAIFA

USHINDI UWE NA MWENDELEZO KIMATAIFA KWA TIMU ZA TAIFA

TABASAMU limeanza kurejea taratibu aada ya timu zetu za Taifa kupata matokeo mazuri kwenye mechi za mwanzo za kirafiki hili ni jambo ambalo linahitaji kuwa na mwendelezo.

Wakiwa Libya, Taifa Stars walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda na Serengeti Boys pia kwenye mchezo wao wa kirafiki walishinda bao 1-0 dhidi ya Sudan  U 17 hawa Serengeti wapo Tanzania.

Wachezaji wa Stars ambao wameweka kambi nchini Libya wana mchezo mmoja mwingine dhidi ya Libya huo nao ni muhimu kupata ushindi.

Kwa wale ambao hawajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa bado wana nafasi kwa kuwa timu ni yetu sote na hakuna mwenye namba ya kudumu katika timu hii.

Kupata ushindi kwenye mechi za kirafiki kuwe ni mwendelezo kwa mechi za ushindani ambazo imekuwa ni ngumu kupata ushindi.

Ukweli ni kwamba Watanzania wanahitaji kuona timu inapata matokeo kwenye mechi za kirafiki na zile za kimataifa ili wawe na shangwe muda wote.

Kwa wale vijana wa U 23 wana kibarua leo kusaka ushindi mbele ya Sudan Kusini kuwania kufuzu AFCON nao mchezo wao wa kwanza walikwama kushinda wakiwa nyumbani wana kazi kubwa kusaka ushindi ugenini.

Ikumbukwe kwamba suluhu ya bila kufungana Uwanja wa Azam Complex kuna makossa ambayo yalionekana nina Imani benchi la ufundi limefanyia kazi na matokeo yatapatikana kwenye mchezo wa marudio.

Umuhimu wa kushinda ni mkubwa na inawezekana kwa kila wakati kufanya maandalizi mazuri na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

Ukiachana nao pia Timu ya Taifa ya Wanawake Serengeti Girls nao wana kazi kubwa ya kufanya kwenye Kombe la Dunia nchini India.

Kila mmoja anajua kwamba Serengeti Girls huwa wanapata matokeo mazuri kwenye mechi za ugenini lakini hili ni Kombe la Dunia hivyo wanakwenda kukutana na ushindani mwingine kabisa.

Inawezeka ikiwa kila mchezaji atajituma kwenye kusaka ushindi uwanjani hapo ni wakati wa kila mmoja kufanya kazi kwa umakini kwa kutimiza wajibu wake.

Mechi zote ambazo wanakwenda kucheza zitakuwa ngumu na itakuwa ni sawa na fainali jambo la muhimu ni kwao pia kufanya maandalizi mazuri.

Kinachohitajika ni matokeo mazuri kwenye mechi zote na inawezekana ikiwa wachezaji watakuwa makini na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.

Imani yetu ni kuona kambi ambazo zinafanyika kwa muda huu pamoja na maandalizi ya mwisho yatakuwa na matokeo mazuri kwa kila mechi ambayo itachezwa.

Kila la kheri wachezaji wetu wa timu za Taifa kazi ni kubwa na tabasamu ni muda wake wa kurejesha kwa Watanzania ambao wanapenda mpira.

Ushindi ni jambo ambalo linahitaji maandalizi na mwendelezo utawafanya mzidi kuwa imara.

Previous articleBURUDANI SAWA, MANDONGA UTANI WAKE USIVUKE MIPAKA
Next articleJEMBE AMPA USHAURI HUU BM 3