Home Sports MECHI MBILI ZA KIRAFIKI SIMBA KUCHEZA ZANZIBAR

MECHI MBILI ZA KIRAFIKI SIMBA KUCHEZA ZANZIBAR

MECHI mbili za kirafiki watacheza wakiwa Zanzibar watanza na Kipanga, Septemba 25 na Septemba 28 watacheza dhidi ya Malindi.

Mechi hizi za kirafiki ni kutokana na mwaliko ambao wameupata kutoka Shirikisho la Soka la Zanzibar, (ZFF).

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa mechi zote zitachezwa saa moja usiku na itakuwa ni maandalizi kwa ajili ya mechi zao za kimataifa.

Simba inatarajiwa kucheza na Clube de Agosto kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika ya nchini Angola.

“Tuna mechi mbili za kirafiki ambazo tutacheza tukiwa huko mchezo wa kwanza utakuwa Jumapili na baada ya siku mbili tutacheza mchezo mwingine Uwanja wa Amaan.

“Baada ya michezo hiyo miwili timu itarejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Agosto,” amesema.

Previous articleLIGI YA MATAIFA YA ULAYA INAENDELEA NA MERIADIANBET WAMEJIPANGA KUTOA PESA KWA AJILI YAKO
Next articleKOCHA MBRAZILI AIBUKIA SIMBA, MASTAA YANGA WAIAPIA AL HILAL