Home Uncategorized KIMATAIFA STARS FANYENI KWELI

KIMATAIFA STARS FANYENI KWELI

MVURUGANO ambao huwa unapatikana baada ya matokeo yasiyotarajiwa kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania kwenye benchi la ufundi pamoja na wachezaji huwa unakuwa sio wa kawaida.

Hii inatokea kwa sababu kila mmoja anapoingia uwanjani mpango wake ni kuona timu inapata matokeo na pale inaposhindikana.

Uzuri ni kwamba mchezo wa mpira ni mchezo wa wazi na makossa yanaonekana kila baada ya dakika 90 kuamilika.

Kwa wachezaji ambao wameshawasili nchini Libya wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanatambua kwamba wana mechi mbili za kucheza ambazo ni za kirafiki.

Hizi ni mechi muhimu kwa kuwa zipo kwenye Kalenda ya FIFA na Septemba 24 wanatarajia kucheza na Uganda kisha watakuwa na mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Libya.

Umuhimu wa mechi hizi ni kwenye kupanda viwango kwenye nafasi ya dunia ina maana kwamba matokeo ya mchezo mmoja ni pointi kubwa inatafutwa.

Makosa ambayo yalitokea kwenye mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Uganda hapo kwenye mchezo huu wa kirafiki ni muda wa kufanikisha kulipa kisasi.

Umakini mkubwa unahitajika na kila mchezaji ana kitu ambacho amejifunza kwa wakati huu ambao ni muda wa maandalizi ya mwisho.

Inawezekana kushinda mechi zote mbili ikiwa wachezaji watakuwa tayari na kujitoa bila kuogopa kwenye mechi zote ambazo watacheza.

Kila la kheri wachezaji ambao mpo nchini Libya kwa ajili ya mechi hizo za kimataifa tunaamini kwamba mtapata matokeo mazuri.

Fanyeni kweli kimataifa Stars kwa kusaka matokeo chanya kwa kuwa ushindi unapatikana kwa kujituma bila kuogopa.

Previous articleSAUTI: MABOSI SIMBA WAMJADILI KOCHA MPYA
Next articleKWA MIPANGO HII YANGA INATOBOA CAF, SIMBA HAKUNA KULAZA DAMU